Submit Your Letter: barua@ppaa.go.tz  Phone:+255743505505       English Swahili  Staff Mail

PPAA2

KARIBU 

Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma  ijulianayo kama PPAA ilianzishwa na Sheria ya Ununuzi ya Umma Na.3 ya mwaka 2001 ambapo baada ya Sheria hii kufutwa, Mamlaka iliendelezwa chini ya Sheria ya Ununuzi ya Umma Na.21 ya mwaka 2004 na kuhuishwa tena kupitia Sheria ya Ununuzi wa Umma Na.7 ya mwaka 2011 baada ya ile Sheria Na.21 ya mwaka 2004 nayo kufutwa.  Kwa mujibu wa Vifungu vya 88(4) na 97 vya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2011, jukumu kuu la Mamlaka ni kupokea, kusikiliza na kutoa maamuzi ya malalamiko au rufaa zitokanazo na maamuzi ya maafisa masuuli katika michakato mbalimbali ya ununuzi wa Umma.  Pia Mamlaka inajukumu la kusikiliza malalamiko yatokanayo na kufungiwa kwa makampuni (blacklisting of tenderers) na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).

diyarbakır escort kartal escort