Uwasilishaji wa Malalamiko au Rufaa

Kuna njia mbili za uwasilishaji wa Malalamiko au Rufaa

 • Njia ya kwanza (Mzabuni   >   Afisa Masuuli   >      PPAA)
 1. Tuma barua rasmi ya malalamiko kwa Afisa Masuuli wa Taasisi ya Umma iliyotanganza zabuni husika ndani ya siku saba (7) za kazi tangua ulipofahamu sababu zinazosababisha malamiko.
 2. Afisa Masuuli atatakiwa kutoa uamuzi wake ndani ya siku saba (7) za kazi.
 3. Ikiwa Mzabuni hajaridhishwa na uamuzi wa Afisa Masuuli au Afisa  Masuuli hajatoa uamuzi ndani ya muda wa siku saba (7) za kazi, wasilisha malalamiko au rufaa mbele ya Mamlaka ndani ya siku saba (7)za kazi toka ulipofahamu jambo au uamuzi unaoulalamikia. Mzabuni awasilishe Malalamiko au Rufaa yake kwa kujaza PPAA Fomu Na. 1 ambayo ni Taarifa ya Rufaa( Bonyeza      kupakua PPAA Fomu 1) pamoja na kulipa ada ya Rufaa(Bonyeza  kuona gharama ).Mamlaka inatakiwa kutoa maamuzi yake ndani  ya siku arobaini na tano(45) tangu kusajiliwa kwa Malalamiko au Rufaa.

 

 • Njia ya pili (Mzabuni   >     PPAA)
 1. Kama mkataba umesainiwa, basi wasilisha malalamiko yako moja kwa moja mbele ya Mamlaka ndani ya siku 7 za kazi toka ulipofahamu jambo hilo.

 ANGALIZO: 

 • Zingatia ukomo wa muda wa uwasilishaji wa Malalamiko au Rufaa mbele ya Mamlaka. Rufaa inapaswa kuwasilishwa ndani ya siku 7 za kazi baada ya kujua jambo au uamuzi unaolalamikiwa.
 • Malalamiko yanayopokelewa ni yale yanayotokana na mchakato wa ununuzi wa Umma kabla ya kutolewa tuzo na yanayohusiana na utoaji wa tuzo kabla ya kusaini mkataba.
 • Mamlaka hii haishughulikii Malalamiko yatokanayo na utekelezaji wa mkataba.

 Mambo yanayoweza kulalamikiwa: -

 • Kukubaliwa au Kukataliwa kwa Zabuni;
 • Tuzo au kusudio la kutoa tuzo;
 • Vipengele visivyokubalika kwenye kabrasha la zabuni;
 • Mchakato wa Zabuni usiozingatia taratibu;
 • Kushindwa au kutokutoa uamuzi ndani ya muda uliowekwa; na
 • Kufungiwa kwa Mzabuni na Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA)

 

 Mawasiliano: -

Katibu Mtendaji,

Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma,

L. P 9310,

DAR ES- SALAAM.

Barua pepe: Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

 

MOTO: Kutoa Maamuzi ya Haki na Kwa Wakati